Kwa mara ya kwanza historia imeandikwa Tanzania baada ya uzinduzi wa Exchange Traded Fund (ETF) ya kwanza kuzinduliwa, mfuko unaoitwa VIS-ETF. Wakati huo huo Orbit Securities kupitia Inuka Fund pia wanaendela kusimama kidedea sokoni.

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa habari na masoko ya fedha Tanzania utakuwa umeisikia VIS-ETF na Inuka Fund. VIS-ETF imekuwa ETF ya kwanza Tanzania, na mauzo ya awali (IPO) yamezidi matarajio kwa asilimia 36%, ikikusanya zaidi ya TZS bilioni 6.8. Wiki ya kwanza pekee, iliuza zaidi ya vipande 700,000.

Wakati huohuo, Inuka Fund kupitia Orbit Securities wamezindua mfuko mpya wa “Dozen Index Fund”, huku Inuka Money Market Fund ikiendelea kuvutia wawekezaji wanaopendelea kuwekeza maeneo yenye hatari (risk) ndogo.

Jiunge na Jamii ya Wasomaji

Kuwa sehemu ya jamii yetu na upate makala mpya, maudhui maalum, na mengi zaidi!

Kuwa Msomaji

Lakini tofauti ni ipi? Na kama una TZS 20,000 tu — ungetakiwa kuwekeza wapi? ili kujibu hili swali kwanza inabidi tuelewe Collective Investment Scheme.

Collective Investment Scheme (CIS)

Mfano rahisi: CIS ni kama daladala ya uwekezaji. Badala ya kununua gari lote (hisa moja kubwa), unalipa nauli kidogo (uwekezaji wako), na dereva (Fund Manager) anakusafirisha pamoja na wengine kuelekea kwenye faida (ukuaji wa soko).

Faida kuu: unapata usimamizi wa kitaalamu na unagawana hatari na wawekezaji wengine.

VIS-ETF ni nini?

VIS-ETF ni mfuko wa uwekezaji unaouzwa kama hisa moja katika soko la DSE), lakini ndani yake kuna “kikapu” cha hisa bora zaidi Tanzania. Ambapo kikapu hicho kinajumuisha hisa zinazofanya vizuri kama CRDB, NMB na NICOL.

Kwanini imepamba vichwa vya habari?

  • Imekuwa IPO ya kwanza ya ETF kwa hapa Tanzania na imeuzwa zaidi (over subscribed) ya ilivyotegemewa kwa asilimia 36%. Kwa maana hiyo imeonekana kuwa na demand kubwa sana.
  • Uwekezaji wa VIS-ETF ni kufuatilia portfolio ya hisa zinazofanya vizuri katika soko la DSE. Kwa maana hiyo ukinunua VIS-ETf moja kwa moja umeisambaza pesa yako katika kampuni zaidi ya tatu tofauti kwa kununua tu ETF moja.
  • Katika IPO yake kiasi cha chini kabisa cha kuwekeza ilikuwa ni Tsh. 20,000 hivyo kuwa wazi kwa mtu wa uwezo wowote kununua hii ETF.

VIS-ETF inamfaa nani?

Kwa muundo wa soko la Tanzania na hii ETF yenyewe inamfaa muwekezaji ambaye anaweka na kusahau. Kwa maana ya kwamba wawekezaji wa muda mrefu. VIS-ETF inawafaa sana wawekezaji wanaotazamia uwekezaji wa miaka 3 au zaidi.

Inuka Fund (Orbit Securities)

Kwanza kabisa ni muhimu kuelewa kwamba Inuka Fund ina mifuko miwili tofauti.

Inuka Money Market

  • Ni nini? Huu ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja ambao unawekeza katika maeneo yenye hatari ndogo ya muda mfupi kama T-Bills na Fixed Bank Deposits. Hii haipo katika orodha ya kampuni zinazouzwa na kununuliwa ndani ya DSE.
  • Lengo ni nini? Lengo ni utunzaji wa fedha na kuwa na stable income. Inuka Money Market inaangalia kuwa juu kidogo ya Treasury bill rate ya siku 364.
  • Data Point. Net Asset Value yake (NAV) ndiyo kitu muhimu. Mpaka kufikia Tarehe 11 November 2025 NAV yake ilikuwa Tsh. 117.18 kwa kila kipande na inaendelea kukua polepole kwa takribani asilimia 12% kwa mwaka.
  • Hii ni kwa ajili ya nani? Kwa muwekezaji anayependa usalama. Ni sehemu nzuri kutunza pesa zenye lengo la dharula au pesa ambayo hauko tayari kuipoteza kwa urahisi. Ni mbadala wa kuwa na account ya kutunzia fedha benki.

Inuka Dozen Index Fund

  • Hii ni index fund mpya kutoka Orbit Securities. Huu ni mfuko unaofuatilia kampuni 12 zinazofanya vizuri ndani ya soko la hisa la DSE.
  • Inuka Dozen Index Fund ni mshindani wa moja kwa moja wa VIS-ETF. Ni mfuko unao onyesha kwamba mameneja wa funds Tanzania wanashindana kuwaletea watanzania njia na namna rahisi zaidi za uwekezaji.
  • Kama ilivyo VIS-ETF, Inuka Dozen Index Fund sio ya muwekezaji wa muda mfupi. Hii inawafaa wawekezaji wa muda mrefu wanao amini katika kampuni ambazo zinafuatailiwa na Inuka Dozen Index Fund.
  • Unaweza kununua Inuka Dozen Index Fund moja kwa moja kupitia Inuka Fund app.

Huu muemko wa uwekezaji sasa hivi ni kitu kizuri kwa Watanzania. VIS-ETF ni njia yako ya kuingia katika kuwekeza katika kampuni mbali mbali za hisa ndani ya soko la DSE. Wakati Inuka Money Market ni mfanyakazi/mlinzi wako wa kukulindia savings zako na mapato madogo madogo unayopata.

Muwekezaji mwenye akili hachagui moja ya kuwekeza bali anawekeza kidogo kidogo katika mifuko yote.